GAZA CITY : Jaribio la tano la suluhu laanza Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 20.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA CITY : Jaribio la tano la suluhu laanza Gaza

Makundi hasimu ya Kipalestina ya Fatah na Hamas yameanza jaribio jipya la kusitisha mapigano huko Gaza likiwa ni jaribio la tano katika wiki moja ya mapigano ambayo yameuwa takriban watu 51.

Mshauri wa Rais wa Palestina Mahmoud Abbas wa kundi la Fatah amesema wapiganaji wameanza kuondoka kwenye mapaa ya nyumba na kuondowa vizuizi barabarani chini ya uangalizi wa wasuluhishi wa Misri.Msemaji wa Waziri Mkuu Ismael Haniyeh amesema makubaliano hayo pia yamejumuisha ahadi kutoka pande zote mbili kuwaachilia mateka inayowashikilia.

Umwagaji damu huo umedhoofisha serikali ya umoja wa kitaifa ya Palestina ambayo imeingia madarakani hapo mwezi wa Machi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com