1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA CITY : Israel yauwa raia 18 wa Kipalestina

8 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCus

Takriban watu 18 wameuwawa wakati vifaru vya Israel viliposhambulia kitongoji cha wakaazi kaskazini mwa Gaza.

Kwa mujibu wa mashahidi wa tukio hilo watu wote waliouwawa wakati wa usiku karibu na mji wa Beit Hanoun walikuwa ni raia wengi wakiwa ni wanawake na watoto.Takriban watu 40 wamekuwa wakipatiwa matibabu katika hospitali.Jeshi la Israel limesema linachunguza repoti hizo.

Baraza la mawaziri la Palestina limetangaza kwamba litaitisha kikao cha dharura kujadili kile ilichokiita kuwa mauaji.

Katika tukio jengine vikosi vya usalama vya Israel vimewauwa wapiganaji wanne wa Kipalestina na raia mmoja katika shambulio karibu na mji wa Ukingo wa Magharibi wa Jenin.