1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA CITY : Afisa mwandamizi wa Fatah auwawa

12 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBsY

Mapigano ya makundi ya wanamgambo wa Kipalestina yamezuka tena katika Ukanda wa Gaza na kuuwa watu 13 akiwemo kiongozi mwandamizi wa kundi la Fatah hapo jana.

Mmojawapo ya waasisi wa kikosi cha Fatah cha Mashahidi wa Al Aqsa Jamal Abu al- Jedian ameuwawa wakati wapiganaji wa Hamas walipovamia nyumba yake huko Beit Lahiya.Watu wengine wanne waliuwawa wakati makundi hasimu ya Hamas na Fatah yalipombana kwenye eneo la hospitali moja kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

Mapema hapo jana Waziri Mkuu Ismail Haniyeh wa kundi la Hamas ilibidi asitishe mkutano wake wa kila wiki wa baraza la mawaziri baada ya risasi kufyatuliwa kwenye jengo lake.

Maafisa wa Hamas wamesema wanaharakati wa Fatah walihusika na ufyatuaji huo wa risasi.