1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gauck : Ujerumani isikwepe wajibu wa kimataifa

23 Februari 2014

Rais Joachim Gauck wa Ujerumani Ijumaa (21.02.2014) amefanya mahojiano na DW katika Kasri la Bellevue mjini Berlin kuhusu sera ya mambo ya nje ambapo amesema Ujerumani haipaswi kukwepa wajibu wake wa kimataifa.

https://p.dw.com/p/1BE8Q
Gauck DW Interview 21.02.2014
Rais Joachim Gauck katika mahojiano ya televisheni na Mkuu wa Studio za DW Berlin Dagmar Engel. (21.02.2014).Picha: Bundespresseamt/Jesco Denzel

Akizungumza katika mahojiano hayo ya televisheni na Mkuu wa Studio za DW Berlin Dagmar Engel amesema huko nyuma kutokana na uhalifu uliofanywa na kizazi cha wazazi wao alikuwa hataki kujitambulisha kama Mjerumani.Lakini Ujerumani imebadilika hatua kwa hatua katika miongo ya hivi karibuni na imekomaa.Gauck amesema" Ujerumani ni nchi tafauti kabisa kuliko ilivyokuwa baina ya wa enzi za vita vikuu vya dunia ".Leo hii anaiangalia Ujerumani hata kwa kuilinganisha na nchi nyengine za Ulaya ambapo anaona hakuna mapungufu ya demokarsia ya kuaminika nchini. Kuna sio tu uzingatifu wa sheria bali pia uwiano wa kijamii baina ya wananchi. Hayo yote yamepelekea Ujerumani ionekane kwa uhakika huko nje kuwa ni mfano wa demokrasia.

Haipaswi kukwepa

Gauck anasema kutokana na mabadiliko hayo Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Ujerumani lazima itambuwe wajibu wake na ikiwa kama nchi kubwa barani Ulaya kwa mfano haipaswi kuchukuwa hatua za kukwepa bali kwa kushirikiana na nchi nyengine za Ulaya ichukuwe dhima ya kushughulikia mzozo wa nchi hiyo.Gauck ameitaka Ujerumani isipuuze kile kinachotokea Ukraine.

Kwa mujibu wa Gauck kuzuwiya mizozo hususan ile inayofanyika chini ya misingi ya kikabila ni wajibu muhimu katika sera ya nje ya Ujerumani. Ametaka Ujerumani pia iangalie hali ya mizozo mengine ilioko mbali katika sehemu nyengine duniani na sio tu Ukraine bali pia katika eneo la Mediterranean na kuona iwapo inaweza kuwa na dhima ya kuwa msuluhishi. Kwa kupitia ushirikiano wa maendeleo wa Ujerumani Rais Gauck amesema katika mahojiano hayo wajibu huo wa Ujerumani pia unahusu kujihusisha kwenye maeneo ya mbali katika masuala ya kulinda mazingira na matumizi ya nishati jadidifu.

Rais Joachim Gauck akihojiwa na Mkuu wa Studio za DW Berlin Dagmar Engel. (21.02.2014).
Rais Joachim Gauck akihojiwa na Mkuu wa Studio za DW Berlin Dagmar Engel. (21.02.2014).Picha: Bundespresseamt/Jesco Denzel

Watu wema wanapoficha silaha zao

Katika hali za dharura wajibu huo wa Ujerumani pia unamaanisha kutuma wanajeshi wake kwa kushirikiana na jumuiya ya kimataifa."Ujerumani hii iliokomaa,ambayo ni mdhamini wa utulivu na demokrasia haiwezi kubakia nyuma" anasema Gauck na kusisitiza kwamba " Si jambo zuri wakati mtutu wa bunduki unapoachiliwa kufanya maamuzi lakini ni jambo baya zaidi wakati watu wema wanapoficha silaha zao na wale walio wabaya wanaachiliwa nazo."

Imedhihirika nini kingelitokea nchini Sebrenica au Rwanda iwapo kungelikuwa hakuna hatua zilizochukuliwa kuingilia kati.Huku sio kujitanuwa kwa maguvu ya Ujerumani bali ni suala la mshikamano.

Rais Joachim Gauck na Mkuu wa Studio za DW Berlin Dagmar Engel. (21.02.2014).
Rais Joachim Gauck na Mkuu wa Studio za DW Berlin Dagmar Engel. (21.02.2014).Picha: Bundespresseamt/Jesco Denzel

Mapema mwezi wa Machi Rais Gauck anapanga kufanya ziara Ugiriki nchi ambayo imeanza kuonyesha ishara za kwanza kurudi kwa utulivu kufuatia mzozo wa madeni. Akiwepo nchini humo atahudhuriya kumbukumbu ya "Historia ya Maovu ya Ujeruman" na pia anatazamiwa kubwaga shutuma kidogo kwani Gauck anaona fedha zinazotolewa na Umoja wa Ulaya kuziokowa nchi zisifilisike na madeni sio mara zote zinatumika kwa ufanisi. Anaona hata Ujerumani inaweza kuisaidia serikali ya Ugiriki ili kwamba iweze kutosheleza viwango vya Umoja wa Ulaya katika matumizi ya fedha za serikali. Anashindwa kuelewa iwapo Kansela Angela Merkel wa Ujerumani inabidi atupiwe lawama kwa mambo yote hayo.

Akiangalia hali ya ndani ya nchi Gauck anakosoa kile anachosema kwamba watu wengi nchini wanahofia uhamiaji. Sanjari na suala hili kuna suala la demografia yenye kuonyesha hali ya jamii fulani na sababu nyingi za kitamaduni anasema "kwa nini tusiweze kufurahia". Kwa hiyo Ujerumani bado haikufikia hasa mwisho wa safari yake ya maendeleo ya demokrasia.

Mwandishi : Naomi Conrad/ Mohamed Dahman

Mhariri : Sudi Mnette