Gadaff kukutana na wabunge wa Ufaransa | Habari za Ulimwengu | DW | 11.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Gadaff kukutana na wabunge wa Ufaransa

PARIS.Kiongozi wa Libya Kanali Mohammar Gadaff anategemwa kukutana na wabunge wa Ufaransa katika siku ya pili ya ziara yake nchini humo.

Wabunge wa upande wa upinzani ambao wa chama cha kisoshalisti wamesema kuwa watagomea mkutano huo na Gadaffi wakisema kuwa ziara ya kiongozi huyo wa Libya imeharibu sifa ya Ufaransa kama mtetezi mkubwa wa haki za binaadamu.

Hapo jana katika siku ya kwanza ziara yake, nchi hizo mbili zilitiliana saini mikataba mbalimbali yenye thamani ya kiasi cha euro billioni 10.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Rais Nicolaus Sarkozy wa Ufaransa, imesema kuwa mikataba hiyo ni pamoja na Ufaransa kuiuzia Libya ndege 21 za abiria aina ya Airbus na makubaliano ya ushirikiano katika nishati ya nuklia kwa matumizi ya kijamii.

Sarkozy ni kiongozi wa kwanza wa nchi za magharibi kumwalika kanali Gadaffi toka kiongozi hiyo alipotangaza kuacha kuunga mkono ugaidi na mpango wa kutengeza silaha za nuklia miaka minne iliyopita.

Kabla ya hapo Libya ilikuwa imetengwa na jumuiya ya kimataifa kwa miongo kadhaa.

Makundi ya haki za binadamu pamoja na waziri wa Ufaransa anayehusika na masuala ya haki za binaadamu, Rama Yade wameshutumu ziara hiyo ya Kanali Gadaffi nchini Ufaransa ambayo ilianza katika siku ya maadhimisho ya haki za binanadamu duniani.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com