Freetown.Mgombea wa tatu kumuunga mkono mgombea wa chama cha upinzani. | Habari za Ulimwengu | DW | 25.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Freetown.Mgombea wa tatu kumuunga mkono mgombea wa chama cha upinzani.

Mgombea kiti cha urais aliyechukua nafasi ya tatu katika uchaguzi mkuu wa Sierra Leone amesema jana Ijumaa kuwa atamuunga mkono mgombea wa chama cha upinzani katika uchaguzi wa duru ya pili unaofanyika baada ya miaka kumi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe katika taifa hilo la Afrika magharibi.

Charles Margai amesema kuwa nia yake ni kuiunganisha nchi hiyo na ndio sababu chama chake kimeamua kumuunga mkono mgombea wa chama cha upinzani cha APC.

Ameongeza kuwa hana nia ya kupata wadhifa wowote wa uwaziri katika serikali ya chama cha APC ama kupata nafasi ya kuwa balozi. Matokeo ya mwanzo kutokana na uchaguzi huo wa August 11 yanaonyesha kuwa kiongozi wa chama cha APC Ernest Koroma amekuwa wa kwanza kwa kupata asilimia 44.3 akimshinda makamu wa rais Solomon Berewa akipata asilimia 38.3. Uchaguzi wa duru ya pili utafanyika mwezi ujao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com