1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Fredericks asimamishwa uwanachama wa IAAF

Bruce Amani
17 Julai 2017

Mwanariadha nyota wa zamani wa mbio za masafa mafupi na ambaye ni mwanachama wa baraza la Shirikisho la Riadha la Kimataifa – IAAF Frankie Fredericks amesimamishwa kwa muda uwanachama wake

https://p.dw.com/p/2gghZ
Frankie Fredericks
Picha: Getty Images/D. Mullan

aadili.

Kitengo cha Uadilifu katika Riadha – AIU cha shirikisho la IAAF kimesema kinachunguza kuhusu malipo yaliyofanywa na kampuni moja inayomilikiwa na Papa Massata Diack – mtoto wa kiume wa aliyekuwa rais wa IAAF Lamine Diack – kwa kampuni moja inayomilikiwa na Fredericks mnamo siku ya au karibu na tarehe ya upigaji kura wa IOC wa kutolewa kibali cha Michezo ya Olimpiki kaundaliwa mjini Rio de Janeiro.

Akiwa mwanachama wa IOC; Mnamibia huyo ambaye sasa ana umri wa miaka 49 aliweza kupiga kura ya kuuchagua mji wa kuandaa michezo ya Olimpiki 2016 wakati uliamuliwa mjini Copenhagen mnamo Oktoba 2, 2009. Mshindi huyo mara nne wa medali za fedha katika Olimpiki awali alijiuzulu kuwa mkuu wa tume ya ukaguzi ya Michezo ya Olimpiki ya 2024, wakati akikanusha madai kuwa alipokea dola 300,000 kutoka kwa la shirika la Ushauri wa Michezo la Pamodzi linalomilikiwa na Papa Massata Diack.

Fredericks alidai kuwa pesa hizo kutoka kwa Pamodzi yalikuwa malipo ya huduma za mauzo alizotoa kati ya mwaka wa 2007 hadi 2011.

Mwandishi: Bruce Amani
Mhariri: Yusuf Saumu