1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FRANKFURT AM MAIN: Madreva wa treni wagoma kazi

6 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7IB

Mgomo uliofanywa siku ya Ijumaa na madreva wa shirika la treni la Ujerumani-Deutsche Bahn ulishindwa kukwamisha huduma zote za usafiri. Shirika hilo la treni lilijiandaa kwa kuajiri madreva wengine na hivyo kupunguza athari za mgomo huo.Umoja wa madreva wa treni-GDL unadai nyongeza ya takriban asilimia 31 na umeonya, migomo mingine itafanywa kuanzia Jumanne ijayo ikiwa maafikiano ya maana hayatopatikana hadi hapo.