FIFA yakanusha kuwa ilimnyima Platini fursa ya kujitetea | Michezo | DW | 12.10.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

FIFA yakanusha kuwa ilimnyima Platini fursa ya kujitetea

Kamati ya maadili ya Shirikisho la Kandanda la Kimataifa imepinga shutuma kutoka kwa rais wa UEFA Michel Platini kuhusiana na namna alivyosimamishwa uongozi, ikisema hoja yake kuwa hakuruhusiwa kujitetea “sio halali”

Platini, alisimamishwa uongozi kwa siku 90 alhamisi iliyopita pamoja na rais wa FIFA Sepp Blatter wakisubiri uchunguzi kamili dhidi yao. Tangazo hilo liliiendeleza kashfa inayolizunguka shirikisho hilo la kandanda la kimataifa.

Taarifa imesema baada ya kitengo cha uchunguzi cha kamati ya maadili kumsikiliza Platini kwa zaidi ya saa tano mnamo Oktoba mosi mwaka huu, ambapo kikao hicho kilichapishwa kwenye nakala zaidi ya 50, mwenyekiti wa kitengo cha maamuzi Hans-Joachim Eckert hakuona haja ya Platini kusikilizwa kwa mara ya pili.

Kwingineko, FIFA imesema leo kwamba rais wa shirikisho la kandanda la Thailand, FAT, Worawi Makudi amepigwa marufuku asijihusishe na shuhguli zote za soka katikangazi ya kitaifa na kimataifa kwa siku 90. Makudi mwenye umri wa miaka 63 ni mwanachama wa zamani wa kamati tendaji ya FIFA na amekuwa rais wa shirikisho la FAT tangu mwaka 2007. FIFA imesema Makundi amepigwa marufuku kwa misingi kwamba inaonekana alikiuka maadili na uamuzi wa suala kuu huenda usichukuliwe mapema.

Taarifa zaidi kuhusu kesi hiyo ambayo sasa itachunguzwa rasmi, hazikutolewa. Mwezi Julai mwaka huu Makudi alihukumiwa kifungo cha nje cha mwaka mmoja na miezi minne baada ya kutiwa hatiani kwa kughushi . Wiki iliyopita FIFA ilipiga marufuku raia Joseph Blatter, katibu mkuu Jerome Valcke na makamu wa rais wa Michel Platini kwa siku 90.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/Reuters
Mhariri: Iddi Ssessanga