1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FIFA yaahirisha mechi ya Ukraine v Scotland

Sylvia Mwehozi
9 Machi 2022

Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limekubali ombi la Ukraine la kuahirisha mechi ya mchujo ya kombe la dunia na Scotland mwezi huu kufuatia vita inayoendelea.

https://p.dw.com/p/48DSw
EURO 2020 | Ukraine vs England
Picha: Alberto Pizzoli/Getty Images/AFP

FIFA imechukua uamuzi huo baada ya mazungumzo na shirikisho la soka barani Ulaya UEFA na kusema "ilikubaliwa kwa pamoja na kwa nia ya mshikamano".

Ukraine ilikuwa imepangwa kuminyana na Scotland katika uwanja wa Hampden Park mnamo Machi 24 katika mechi ya mchujo ambayo sasa itachezwa mwezi Juni.

Mkuu wa shirikisho la soka la Scotland FA , Ian Maxwell amesema huo ni uamuzi sahihi. "Umuhimu wa mpira wa miguu umepungua sana wakati wa vita na mawazo yetu yako kwa raia wa Ukraine walioathiriwa na mzozo," alisema Maxwell.

Mechi ya mchujo ya Wales v Austria itachezwa kama ilivyopangwa-Machi 24. FIFA pia imetangazwa kuwa Poland iliyokuwa ikutane na Urusi katika mechi ya mchujo itasonga mbele na kumsubiri mshindi katika ya Sweden v Czech Republic Machi 29.

Urusi iliondolewa katika mechi za kufuzu kombe la dunia wiki iliyopita baada ya kusimamishwa katika mashindano yote ya kimataifa na FIFA sambamba na UEFA.