FIFA: Niersbach hana makosa yoyote | Michezo | DW | 13.03.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

FIFA: Niersbach hana makosa yoyote

Rais wa Shirikisho la Kandanda la Ujerumani – DFB Wolfgang Niersbach ameondolewa makosa yoyote ya kimaadili na Shirikisho la Kandanda Ulimwenguni – FIFA kuhusiana na malipo na pensheni yake

Inafuatia malalamiko yaliyowasilishwa na mwanachama wa kamati kuu ya FIFA Theo Zwanziger, ambaye ni mtangulizi wa Niersbach kama Rais wa DFB.

Taarifa ya FIFA imesema uchunguzi wa mwanzo wa kamati ya maadili “umekuta kuwa hakuna sheria yoyote ya FIFA kuhusu maadili ambayo imekiukwa katika suala hilo”.

Kamati ya maadili ilichunguza mapato ya pensheni ya Niersbach na rekodi za malipo yake kama ilivyoombwa na Zwanziger mnamo Februari 10.

Hivyo basi jopo la uchunguzi limelifunga suala hilo. Niersbach amekuwa rais wa DFB tangu Zwanziger alipojiuzulu kutoka wadhifa huo baada ya miaka minane mnamo mwaka wa 2012. Anataka kuchukua nafasi ya Zwanziger katika kamati kuu ya FIFA wakati Zwanziger atakapoondoka Mei 29 katika mkutano mkuu wa FIFA.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reuters
Mhariri:Gakuba Daniel

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com