1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FIFA kujadiliana kuhusu Kombe la Dunia

Grace Kabogo
21 Mei 2021

Baraza kuu la shirikisho la soka ulimwenguni, FIFA linafanya mkutano wake huku hoja inayotarajiwa kuhanikiza ikiwa ni pendekezo la michuano ya kombe la dunia kufanyika kila baada ya miaka miwili badala ya minne kama ilivyo sasa. Pendekezo hilo limewekwa kwenye ajenda ya mkutano wa kilele wa baraza hilo na Shirikisho la Soka la Saudi Arabia ambalo liko karibu na rais wa FIFA Gianni Infantino.

https://p.dw.com/p/3tmo0

Maswali mengi yanaibuka kuhusiana na pendekezo hili, ambalo kwa kiasi kikubwa linakosolewa na baadhi ya wadau. Je wadau wa michezo wanalionaje pendekezo hilo? Hilo ni miongoni mwa maswali ambayo Lilian Mtono amemuuliza mwanahabari mwandamizi Sekione Kitojo.