1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FDP: Kiongozi Christian Lindner aotea kurudi bungeni

Zainab Aziz
25 Agosti 2017

Chama cha FDP kilishindwa katika uchaguzi miaka minne iliyopita.Chiristian Lindner anakiongoza tena chama chake katika uchaguzi wa Septemba 24. Kwenye mahojiano na DW alizilaumu sera za kansela Angela Merkel.

https://p.dw.com/p/2iriH
Ines Pohl und Jaafar Abdul-Karim interviewen Christian Lindner für die Deutsche Welle
Picha: DW/Ronka Oberhammer

Huku uchaguzi mkuu wa hapa Ujerumani ukiwadia, kiongozi wa chama cha Kiliberali ameilaumu sera ya Kansela Angela Merkel kuhusu wakimbizi kuwa inazorota sana. Kiongozi huyo wa chama cha FDP, Christian Lindner, anasema chama chake kina sera bora zaidi kuhusu wakimbizi na wahamiaji.

Kiongozi huyo wa chama cha kiliberali, Christian Lindner, amesema inachukua muda mrefu kuyashughulikia maombi ya kutaka hifadhi chini ya sera za kansela Angela Merkel na badala yake yeye anaifanyia kampeni sera ya uhamiaji ya ''milango Minne''.  Lindner ansema Ujerumani inapaswa kubadili mtazamo wake. Makakati wa Lindner wa kampeni za kuwania ukansela kwa niaba ya chama chake cha FDP katika uchaguzi wa tareehe 24 mwezi Septemba ni pamoja na kujitenga na kuendelea kuwepo kwa wanajeshi wa Ujerumani nchini Afghanistan.

Mgombea huyo wa ukansela kwa niaba ya chama cha kiliberali mwenye umri wa miaka 38 hakutafuna maneno yake hata kidogo pale alipozungumzia juu ya uhusiano wa Ujerumani na Uturuki Lindner alisisitiza kuwa uhusiano wowote wa kibiashara baina ya nchi hizo mbili usimaishwe mara moja.  Lindner alizungumzia kuhusu matukio kadhaa yaliyofuatia jaribio la kuipindua serikali ya Uturuki lililoshindikana la mwaka uliopita wa 2016. Baada ya jaribio hilo la mapinduzi, maelfu ya watu nchini humo wamekamatwa na kufungwa jela. Vile vile kiongozi huyo wa chama cha FDP amezungumzia juu ya kubinywa kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini Uturuki.

Christian Lindner pia ameilaumu vikali sera ya Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kuhusu wakimbizi na amependekeza kuwepo hifadhi ya muda inayozingatia masuala ya kibinadamu ili kuuharakisha mchakato wa kuomba hifadhi nchini Ujerumani. Amesema kwamba katika mapendekezo yake ingefaa ikiwa wakimbizi watapewa vibali vya kuishi na ambavyo vitawaruhusu mara moja kutafuta ajira na mara amani itakaporejea katika nchi wanazotoka basi watalazimika kurudi kwenye nchi zao. Mapendekezo hayo ni hatua mojawapo ya sera za chama chake juu ya masuala ya uhamiaji.

Katika mahojiano na mhariri mkuu wa DW, Ines Pohl, kiongozi huyo wa chama cha kiliberali alisisitiza kuwa malengo yaliyowekwa na serikali ya Kansela Merkel kuhusu Afghanistan bado hayajafanikiwa na kwamba labda malengo hayo yaliyokusudia kuifanya Afghanistan kuwa na demokrasia yalifikiwa katika misingi ya tamaa tu.  Chama hicho cha FDP kwa sasa hakiwakilishwi bungeni lakini iwapo chama hicho kitapata viti vya kutosha kukiwezesha kuingia katika ushirikiano wa muungano wa vyama, Lindner anataka kurudi kwenye hali anayoiita Ujerumani ya Jadi.

Deutschland wählt DW Interview mit Christian Lindner
Kulia ni Christian Lindner, akihojiwa na mhariri mkuu wa DW Ines Pohl, kushoto, na mwandishi wa DW Jaafar Abdul Karim.Picha: DW/R. Oberhammer

Christian lindner pia katika mahonjiano hayo aligusia juu ya kauli yake iliyozua utata kuhusu haua ya Urusi ya kulikata jimbo la Crimea. Lindner awali aliliambia gazeti la Westdeutsche Allgemeine kwamba ingawa hatua hiyo ya Urusi imekiuka misingi ya sheria za kimataifa lakini inapaswa kuchukuliwa kama hatua ya kudumu na pia aliilaumu Ujerumani na sera zake kauli ambayo ilizusha malalamiko ndani ya Ujerumani.

Matokeo ya uchaguzi na baadae majadiliano ya kuunda serikali ya ushirikiano katika muungano wa vyama ndio yataamua kama chama hicho cha FDP kinachoongozwa na Christian Lindner iwapo kitaweza kuyatekeleza mawazo yake katika serikali ijayo ya Ujerumani. Kwa sasa, matokeo ya kura ya maoni kabla ya uchaguzi yanaonyesha kuwa chama cha FDP kina asilimia 8 - sawa na chama cha kijani na pia chama Afd kinachojulikana kama cham Mbadala kwa Ujerumani. Chama kinachoehgemea mrengo wa Kushoto kina asilimia 9.

Hadi sasa hakuna chama kati ya hivyo kinachoweeza kushikilia nafasi ya tatu  ambacho kinaweza kuwa na nafasi ya kuunda serikali na chama cha Christian Democratic Union CDU kinachoongozwa na kansela Angela Merkel pamoja na chama ndugu cha Christian Social Union CSU katika bunge la Ujerumani, Bundestag. Katika wiki za hivi karibuni, Lindner mara nyingi amesema kuwa upo uwezekano wa yeye kuwa na nafasi muhimu katika upinzani kwenye siasa za hapa Ujerumani naanweeza kuchukua nafasi ya kuwa kiongozi wa upinzani.

Mwandishi: Zainab Aziz/Rupert Wiederwald
Mhariri: Mohammed Khelef