FBI wahudhuria kesi ya Sudan Kusini | Matukio ya Afrika | DW | 06.06.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

SUDAN KUSINI

FBI wahudhuria kesi ya Sudan Kusini

Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) linahudhuria siku ya pili ya kusikilizwa kesi dhidi ya wanajeshi wanaotuhumiwa katika mashambulizi mabaya kabisa dhidi ya wafanyakazi wa kigeni nchini Sudan Kusini.

Wanaume 12 wanatuhumiwa kwa ubakaji, mateso na mauaji katika shambulio la mwezi Julai katika hoteli ya Terrain ilioko katika mji mkuu wa Sudan Kusini Juba.

Marekani imetoa msaada kwa ajili ya uchunguzi huo na msemaji wa ubalozi wa Marekani amesema uwepo wa FBI nchini Sudan Kusini umetokana na majadiliano.

Serikali ya Sudan Kusini inasema Marekani imetoa msada wa kiufundi na kiuchunguzi kuwabaini watuhumiwa.

Mahakama leo imekataa ombi la upande wa mashitaka la mapunmziko ya mwezi mmoja ili kujiandaa zaidi.

Wengi wa waathirika wa kisa hicho wanaishi nje ya nchi.

Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com