FBI sasa yamchunguza Sepp Blatter | Michezo | DW | 07.12.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

FBI sasa yamchunguza Sepp Blatter

Maafisa wa Marekani wanachunguza ushahidi unaoonesha kwamba rais wa shirikisho la kandanda duniani FIFA aliyesimamishwa kazi kwa muda Sepp Blatter anafahamu juu ya dola milioni 100 zilizotolewa kama hongo kwa wajumbe

Uchunguzi wa kituo hicho cha utangazaji nchini Uingereza unadai kwamba kampuni ya kuuza matangazo ya ISL imelipa jumla ya dola milioni 100 kwa maafisa ikiwa ni pamoja na rais wa zamani wa FIFA Joao Havelange na mkuu wa zamani wa FIFA Ricardo Teixeira. Kwa hongo hiyo kampuni hiyo ilipata haki za kutangaza na kuuza matangazo hayo katika miaka ya 1990, ripoti hiyo imesema. Blatter anaendelea kudai kwamba hakufahamu kuhusu malipo hayo, lakini uchunguzi huo umesema umeona barua iliyopatikana na shirika la uchunguzi wa makosa ya jinai nchini Marekani FBI ambayo inatilia shaka juu ya kukana kwake.

Wakati huo huo wachezaji wa kandanda nchini Brazil walionesha upinzani wao dhidi ya viongozi wa chama cha mpira wa miguu nchini Brazil jana.

Wachezaji walioteremka katika viwanja mbali mbali nchini Brazil jana walifunga mikono yao na kusimama kwa kutulia kwa muda mfupi mwanzoni mwa michezo ya ligi ya Brazil Serie A wakidai kujiuzulu kwa Marco Polo Del Nero, rais wa shirikisho la kandanda la Brazil CBF ambaye anashitakiwa na maafisa wa Marekani.

Del Nero , amechukua likizo ya kutokuwapo kazini kupambana na madai dhidi yake na anadai kwamba hana hatia. Ni rais wa tatu wa CBF kushitakiwa ama kukamatwa mwaka huu.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre / afpe / ape / dpae
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com