1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Familia ya Patrice Lumumba yapambana kutafuta haki Ubelgiji

21 Januari 2026

Kwa miaka 15 iliyopita familia ya waziri mkuu wa kwanza wa Kongo huru, Patrice Lumumba imekuwa ikishinikiza kufanyika kile inachosema ni, haki ya kisheria, kuwashtaki maafisa wa Ubelgiji waliohusika na mauaji ya Lumumba

https://p.dw.com/p/57Aak
Juliana Lumumba, Binti wa Patrice Lumumba akiwa pamoja na jamaa wa familia
Juliana Lumumba, Binti wa Patrice Lumumba akiwa pamoja na jamaa wa familia Picha: Bashi Wendy/DW

Familia ya aliyekuwa waziri mkuu wa kwanza wa Kongo Huru, Patrice Lumumba, imesema ina matumaini ya kupata haki kufuatia hatua ya Mahakama ya Ubelgiji kufikiria kumfungulia mashtaka mshukiwa pekee aliyebakia wa mauaji ya kiongozi huyo mnamo mwaka 1961.

Genge la wahalifu lavamia makumbuyho ya kaburi la Lumumba DRC

Kwa miaka 15 iliyopita familia ya Lumumba imekuwa ikishinikiza kufanyika kile inachosema, haki ya kisheria dhidi ya maafisa wa Ubelgiji waliohusika kwenye mauaji ya mwanasiasa huyo maarufu.

Etienne Davignonmwenye umri wa miaka 93, aliyewahi wakati mmoja kuwa kamishna wa Umoja wa Ulaya alikuwa mwanadiplomasia wa Ubelgiji wakati wa mauaji ya Lumumba yaliyofanywa miaka 65 iliyopita na mamluki kutoka Ubelgiji.