1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FALLUJAH:Watu tisa wauwawa kwenye shambulio la Bomu

28 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVK

Mshambuliaji wa kujitoa muhanga aliyekuwa amejifunga mkanda wa milipuko amejiripua miongoni mwa waumini jana jioni katika eneo la Falujjah na kuua watu 9 akiwemo imamu wa msikiti ambaye alikuwa akikashifu vitendo vya kundi la Alqaeda.

Kwa mujibu wa Polisi watu wengine kumi walijeruhiwa katika tukio hilo lililotokea kwenye msikiti wa Raqeeb kaskazini mwa mji wa Falluja,Inaaminika kuwa shambulio hilo lilikuwa limekusudiwa kumuua imamu huyo Abdul Sattar al Jumaili ambaye wanawe wawili waliuwawa.Al Jumaili ameuwawa siku moja baada ya kuwasili Iraq kutoka Syria.

Wakati huo huo waumini wakishia waliokuwa na hasira juu ya kuwekwa sheria kali za usalama katika sherehe za kidini walipambana na polisi na watu watatu kuuwawa katika mji wa Karbala.

Mamia kwa maelfu ya waumini wakishia walikusanyika katika mji wa Melee kusherehekea maadhimisho ya siku ya kuzaliwa ya imam wa mwisho wa mashia Mohammed al-Mahdi aliyetokweka katika karne ya tisa.

Serikali iliweka sheria za kuwapekua watu kufuatia matukio ya mashambulizi yanayofanywa mara kwa mara na wanamgambo wa kisuuni katika sherehe kama hizo.