Fainali Champions League yahamishiwa Porto kutoka Istanbul | Michezo | DW | 13.05.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Fainali Champions League yahamishiwa Porto kutoka Istanbul

Mechi ya fainali ya michuano ya Champions League baina ya Manchester City na Chelsea itakayochezwa Mei 29, imehamishiwa mjini Porto Ureno, kutoka Istanbul nchini Uturuki kwasababu ya janga la virusi vya corona.

Shirikisho la mpira wa miguu barani Ulaya UEFA, limesema katika taarifa yake hii leo. Ni mwaka wa pili sasa mfululizo Istanbul inashindwa kuandaa michuano ya kimataifa kama ilivyopanga kutokana na janga la corona na kuilazimu Ureno kuingilia kati.

Uamuzi huo umechangiwa na hatua ya Uingereza kuiweka Uturuki katika orodha yake ya nchi hatari kwa wasafiri kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona. Mashabiki wapatao 6,000 kutoka kila timu wataruhusiwa kushuhudia fainali hizo.

Ureno imo katika orodha ya nchi salama kwa wasafiri ikimaanisha kwamba hakuna kipindi cha karantini kwa wale watakaorejea.