F1: Hamilton azawadiwa ushindi nchini Bahrain | Michezo | DW | 01.04.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

F1: Hamilton azawadiwa ushindi nchini Bahrain

Ushindi wa kushangaza wa Lewis Hamilton na timu ya Mercedes katika mbio za Bahrain Grand Prix Jumapili ndio zawadi ya karibuni kabisa kutolewa na wapinzani wao wa Ferrari

Hamilton alishinda licha ya kuwa nyuma ya madereva wa Ferrari kwa kipindi kirefu cha mbio hizo. Kwanza Sebastian Vettel alikabiliwa na shinikizo na gari lake likapoteza muelekeo. Kisha mambo yakawa mabaya hata Zaidi kwa Ferrari baada ya injini ya gari la kiongozi wa mbio hizo Charles Leclerc kuanza kupoteza umeme.

Leclerc alimaliza katika nafasi ya nne nyuma ya Valtteri Bottas wa Mercedes wakati timu hiyo ikishinda nafasi mbili za kwanza katika mbio mbili za msimu huu. Mwshowe, Hamilton alimpa pole Leclerc n ahata kumsifia

Max Verstappen wa timu ya Red Bull alimaliza wa nne huku Mjerujamani Vettel akinyakua nafasi ya tano