F1: Hamilton ashinda mahsindano ya Mexico | Michezo | DW | 28.10.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

F1: Hamilton ashinda mahsindano ya Mexico

Lewis Hamilton alipata ushindi sherehe ya ushindi wa mkondo wa Mexico alioutamani sana. Lakini atalazimika kusubiri kwa wiki nyingine ili kupata ubingwa wake wa sita wa ulimwengu.

Dereva huyo wa timu ya Mercedes aliwapiku madereva wa Ferrari na kushinda mbio za Mexican Grand Prix jana, na kusogea karibu na ubingwa wa msimu ambao ulimhakikishia kushinda taji la dunia wiki ijayo katika mashindano ya US Grand Prix jimboni Texas.

"Hizi ni mbio nilizotamani kushinda kwa muda sasa na kawaida imekuwa vigumu kwetu. kwa hiyo nimefurahishwa sana na fursa ya leo na kwa gari kuwa katika hali nzuri na timu yangu kuweka mkakati bora kabisa." Alisema Muingereza huyo

Sebastian Vettel wa Ferrari alimaliza wa pili huku dereva mwingine wa Mercedes Valtteri Bottas akipanda jukwaani katika nafasi ya tatu