F1: Hamilton ampiku Vettel Uhispania | Michezo | DW | 15.05.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

F1: Hamilton ampiku Vettel Uhispania

Katika mbio za magari ya Formula One, dereva Lewis Hamilton alirejea jana kwa kishindo katika kujaribu kuwinda taji la nne la dunia wakati aliipa timu yake ya Mercedes ushindi wa mbio za Spanish Grand Prix

Bingwa huyo mara tatu alianza vibaya baada ya kupokonywa uongozi na dereva wa Ferrari Mjerumani Sebastian Vettel ambaye alimaliza wa pili naye Muastralia Daniel Ricciardo wa Red Bull akamaliza wa tatu.

Ulikuwa ushindi wa pili wa Muingereza Hamilton kati ya mbio tano mwaka huu na wa 55 katika taaluma yake na sasa yuko  nyuma ya Vettel na pengo la pointi sita katika kiyang'anyiro cha ubingwa wa dunia. Vettel ana pointi 104 na Hamilton ana 98.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Iddi Ssessanga