EU kuwa bega kwa bega na Kosovo | Habari za Ulimwengu | DW | 20.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

EU kuwa bega kwa bega na Kosovo

NEW YORK.Umoja wa Ulaya umesema kuwa utakuwa mstari wa mbele kuhakikisha majaaliwa ya hadhi ya jimbo la Kosovo.

Tamko hilo limekuja baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo jana kushindwa kufikia muafaka juu ya suala la kutaka kujitenga kwa jimbo la Kosovo kutoka Serbia.

Serbia na Urusi zimelitaka baraza hilo kuandaa mazungumzo zaidi juu ya suala hilo.Lakini wawakilishi wa Umoja wa Ulaya na Marekani wamesema kuwa hatua za kutafuta suluhisho la suala hilo kwa njia ya majadiliano zinachosha.

Waziri Mkuu wa Serbia Vojislav Kostunica kwa upande alisema kuwa nchi yake kamwe haitokubali azimio la kuipatia uhuru Kosovo na kuzusha wasi wasi wa kurejea kwa ghasia katika eneo hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com