Ethiopia yapoteza hadhi yake kwa mataifa fadhili ya magharibi, kutokana na ukandamizaji. | Matukio ya Kisiasa | DW | 30.01.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Ethiopia yapoteza hadhi yake kwa mataifa fadhili ya magharibi, kutokana na ukandamizaji.

Hadhi ya Ethiopia ya kile kinachoitwa kipenzi cha wafadhili imepungua kutokana na ukandamizaji dhidi ya uhuru wa habari pamoja na wapinzani wa kisiasa.

Makao makuu ya umoja wa Afrika mjini Addis Ababa wakati wa mkutano wa kumi wa umoja huo.

Makao makuu ya umoja wa Afrika mjini Addis Ababa wakati wa mkutano wa kumi wa umoja huo.

Ilikuwa wakati wa hali mbaya kabisa ya njaa katika miaka ya 70 na 80, hadhi ya Ethiopia ya kile kinachoitwa kipenzi cha wafadhili iliasisiwa. Kujiingiza kwa nchi hiyo lakini katika siku za hivi karibuni kijeshi nchini Somalia kumeiangusha nchi hiyo, kisiasa, kwa upande wa mataifa ya magharibi, na kwamba haikuwa tayari kubeba mzigo wa operesheni ya kijeshi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Somalia. Na Umoja wa Afrika ambao una makao yake makuu katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa , unasikitishwa kuwa matokeo ya kisiasa pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo si suala linalopewa umbele.Na sasa inaonesha kuwa serikali imefika mbali zaidi. Baada ya kukamatwa tena kwa kiongozi wa upinzani na kuanzishwa sheria kali dhidi ya asasi zisizo za kiserikali Washirika wa Ethiopia, mataifa ya magharibi, kwa mara ya kwanza wametoa matamshi ya kukosoa na yanafikiria kuiwekea zaidi vikwazo.

Mara tu baada ya uchaguzi uliogubikwa na umwagaji damu mwaka 2005, wafadhili wa Ethiopia walisitisha kutoa misaada, wakionyesha upinzani wao kwa kuacha kutoa msaada katika bajeti ya nchi hiyo. Na msaada huo kuwekwa katika kile kinachoitwa ulinzi wa huduma za msingi, ikiwa ni pamoja na madawa pamoja na mpango wa elimu.

Baada ya kukamatwa kiongozi wa upinzani, Birtukan Medeksa, ambaye kwa muda amewekwa katika kizuizi cha nyumbani, na pia huenda akafungwa maisha pamoja na kuwekwa sheria kali dhidi ya asasi zisizo za kiserikali mwanzoni mwa mwaka huu , washirika wa Ethiopia wanafikiria kwa kweli kufuta kabisa hata msaada huu wa kifedha.

Serikali ya Ethiopia , kutokana na hali kwamba ina upungufu mkubwa wa fedha za kigeni na kwamba kwa kiasi kikubwa haina fedha kabisa, itaathirika mno.

Utawala wa Ethiopia mjini Addis Ababa unatetea kukamatwa tena kwa Birtukan, ambaye alikamatwa wakati wa uchaguzi mwaka 2005 na mwanzoni mwa mwaka jana aliachiliwa huru, akiwekewa masharti magumu, kinyume na utaratibu wa katiba.

Ato Shimeles Kemal, alikuwa mwanasheria mkuu wa serikali 2005, na alidhibiti kesi za wapinzani na kiongozi huyo wa kundi la kutetea haki za binadamu.

Katika miezi ya Juni na Oktoba 2005, kundi la watu lilijaribu kuiangusha serikali kwa nguvu na kuiondoa katiba kwa nguvu. Matumizi haya ya nguvu yamesababisha watu wengi kupoteza maisha yao, Wanausalama , ambao walikuwa wakijaribu kurejesha utulivu, waliuwawa. Kutokana na msingi huu , wapinzani, kama Birtukan Medeksa, wamekiri kuwa wana makosa na walihukumiwa adhabu ya kifungo cha nje cha maisha.


Washirika wa Ethiopia wa mataifa ya magharibi walikuwa na maelezo tofauti katika hali hiyo ya matukio. Kwa mujibu wa wale waliofyatuliwa risasi ni kwamba baada ya ushindi wa upinzani katika uchaguzi polisi walifyatua risasi kila mahali, na hukumu dhidi ya wanaharakati ilikuwa tu kama mchezo wa kuigiza, ambapo ni muendelezo wa kukamatwa tena kwa mwanaharakati Birtukan.

Mbunge wa Ureno Anamaria Gomes aliongoza 2005 ujumbe wa umoja wa Ulaya ulioangalia hali nchini Ethiopia.

Hii inaoana moja kwa moja na utaratibu wa ukandamizaji wa utawala huu wa Meles Zenawi. Nafahamu kuwa hali ni ngumu sana nchini Ethiopia, kuna ukandamizaji wa uhuru wa vyombo vya habari, uingiliaji kati wa serikali kutoa maelezo yasiyo sahihi katika utaratibu wa kidemokrasi kwa wananchi na kueleza mfumo bandia wa uchaguzi ambao Meles Zenawi, bila shaka atakuwa mshindi.


Kama mmoja wa washirika wake wakubwa katika maendeleo, serikali ya Ujerumani pia imetoa malalamiko yake kwa Ethiopia. Mjumbe wa tume ya haki za binadamu katika bunge la Ujerumani Günter Nooke , ameikosoa sana serikali ya Ethiopia wakati wa ziara yake ya hivi karibuni mjini Addis Ababa na kudai utekelezaji.
 • Tarehe 30.01.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GkCV
 • Tarehe 30.01.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GkCV
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com