1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

E.Terreblanche na kifo chake .

6 Aprili 2010

Afrika Kusini yaelekea wapi ?

https://p.dw.com/p/MoFS
Jacob Zuma:vipi kuzuwia machafuko yasitokee ?Picha: picture-alliance/dpa

Maoni ya wahariri wa magazeti ya leo ya Ujerumani ,yametuwama hasa juu ya mada mbili : athari za kuuwawa kwa Terreblanche,kiongozi wa wazungu aliekuwa na siasa kali enzi za "apartheid " -ubaguzi na mtengano -kwa usalama wa nchi hii-wiki chache kabla kuanza kwa Kombe la dunia.Mada ya pili ni vita vya umwagaji damu nchini Afghanistan pamoja na Jeshi la Ujerumani huko Afghanistan.

Gazeti la Fuldaer Zeitung, juu ya kuuwawa kwa Eugene Terreblanche, nchini Afrika kusini laandika:

"Mara nyingi , cheche za moto zinatosha kuzusha mripuko mkubwa.Na nchini Afrika kusini, kuuwawa kwa kaburu aliekuwa na siasa kali Terreblanche, yamkini ikawa ni chche yenyewe.

Maoni ya kambi mbali mbali, yamebainisha dhahiri-shahiri kuwa, ugomvi wa kikabila humo nchini , bado haukumalizika na Bw.Zuma pamoja na chama cha Upinzani cha Democratic Alliance, anafanya kila kinachowezekana ili kutotumiwa kisiasa kitendo cha kihalifu kilichotokea lakini pia kwa sehemu kubwa, kutowachafulia mashabiki wa dimba Kombe la dunia."

Ama gazeti la Berliner Zeitung, linaandika kwamba, mauaji yaliozuka wiki 10 kabla ya Kombe la dunia, yana baruti za kuripua balaa la kikabila lililojificha nyuma ya pazia la "Rainbow Nation" -Taifa la makabila mbali mbali kutokana na chuki za kikabila na hali mbaya za kijamii.Gazeti laongeza:

"Kisa halisi hapa ,ni sauti za kichochezi za wanamgambo wa ANC wanaoimba nyimbo za chuki: "mueni kaburu".Muimbaji nyimbo hiyo ni Julius Malema,kiongozi wa chama cha vijana cha chama-tawala cha ANC.Malema , alikuwa jana ziarani nchini Zimbabwe na anapongeza siasa za rais Robert Mugabe......"

Ni kiroja cha mambo, laandika gazeti la (SHWEBISHE ZEITUNG) Schwäbische Zeitung kuona imesadifu kifo cha mbaguzi Terreblanche kinachotoa fursa kwa uongozi wa kisiasa nchini kuthibitisha kukomaa kwa demokrasia nchini.IGazeti laongeza :

Inafanyika hivyo kwa njia ambayo, viongozi karibu na rais Jacob Zuma , wanajitahidi kuona, wauaji wanakabili adhabu kali ya kisheria.Kuona kwamba, sheria inatumika bila ya ubaguzi na hata kwa wale maadui wa dola linalofuata kisheria.

Likitugeuzia mada,gazeti la Ostsee-Zeitung (OSTZII-SEITUNG) linachambua ijumaa DPAya pasaka ya bahari ya damu nchini Afghanistan, ambamo askari zaidi wa Ujerumani (Bundeswehr) ,walijeruhiwa na wanajeshi-shirika 6 wa kiafghanini, waliuwawa kwa makosa. Gazeti laandika:

"Kisa hiki , kimefufua upya mjadala juu ya kushiriki kwa wanajeshi wa Ujerumani katika vita vya Afghanistan.Mvutano kati ya wale wanaopinga na wanaoungamkono, umefikia kilele chake katika swali: Je, warudi nyumbani au wabakie huko ?

Kufunga virago sasa na kurudi nyumbani , maana yake ni kusalim amri mbele ya waislamu wa enzi za kale ambao wanachukiza kwa sehemu kubwa ya waafghani.Wakibakia , ndio kukabili mtihani uliopo .Kwa jukumu la hatari waliopewa wanajeshi wa Ujerumani huko Afghanistan, wanastahiki kuoneshwa mshikamano nao hapa nyumbani-Lamaliza gazeti.

Mwandishi: Ramadhan Ali/ DPA

Uhariri: O.Miraji