ESSEN : Ujerumani yataka kutanuliwa Kundi la Mataifa Saba | Habari za Ulimwengu | DW | 10.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ESSEN : Ujerumani yataka kutanuliwa Kundi la Mataifa Saba

Waziri wa Fedha wa Ujerumani Peer Steinbrück amesema anapendelea kutanuliwa kwa Kundi la Mataifa Saba yenye maendeleo makubwa ya viwanda duniani kwa kuzijumisha nchi za Urusi na China.

Wito huo umekuja kwenye mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa fedha kutoka mataifa saba yalio tajiri kabisa duniani. Pia katika mkutano huo wa Kundi la Mataifa Saba katika mji wa Essen nchini Ujerumani nchi za Marekani,China pamoja na Ujerumani zimeelezea shauku yao ya kutaka kuanzishwa tena kwa mazungumzo ya biashara duniani yaliokwama katika wiki za hivi karibuni.

Kile kinachojulikana kama Duru ya Doha mazungumzo ya Shirika la Biashara Duniani WTO ya mwaka 2001 yanayolenga kuimarisha masharti ya biashara kwa nchi zinazoendelea yamekwama tokea mwezi wa Julai mwaka jana.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com