1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Eriksson afariki dunia

26 Agosti 2024

Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya England Sven-Goran Eriksson amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76 baada ya kuugua saratani.

https://p.dw.com/p/4jvwl
Kocha wa zamani wa England Sven-Goran Eriksson
Kocha wa zamani wa England Sven-Goran ErikssonPicha: Khaled Desouki/AFP/Getty Images

Haya ni kwa mujibu wa wakala wake Bo Gustavsson. Eriksson aliyekuwa raia wa Sweden, ndiye kocha wa kwanza wa kigeni kuifunza timu ya taifa ya England.

Aliiongoza timu ya England ilipokuwa na wachezaji mahiri kama David Beckham, Frank Lampard, Steven Gerard, Paul Scholes na Wayne Rooney.

Eriksson ambaye aliziongoza timu za Sweden, Ureno na Italia kunyakua mataji katika miaka ya 1980 na 1990 kabla kuchukua uongozi wa England mwaka 2001, alitangaza mapema mwaka huu kwamba anaugua saratani ya kongosho.