ERFURT : Wakumbuka mauaji ya shule ya mwaka 2002 | Habari za Ulimwengu | DW | 27.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ERFURT : Wakumbuka mauaji ya shule ya mwaka 2002

Jana kulifanyika kumbukumbu ya mauaji ya shule yaliotokea miaka mitano iliopita katika mji wa Erfurt nchini Ujerumani.

Kengele zililia na watu waliweka maua mbele ya eneo la kumbukumbu la wahanga wa maafa hayo.Hapo mwaka 2002 mwanafunzi wa zamani wa Shule ya Sekondari ya Gutenberg aliwapiga risai na kuwauwa wanafunzi wawili, wafanyakazi 13 wa shule na polisi mmoja na baadae kujiuuwa yeye mwenyewe.

Maafisa wa shule wanasema kiwewe cha mauaji hayo holela mabaya kabisa kuwahi kushuhudiwa nchini Ujerumani baada ya kipindi cha vita kimeamshwa hivi karibuni kutokana na mauaji ya chuo kikuu cha Virginia nchini Marekani.

Wengi ya wale walionusurika katika mauaji ya Erfurt bado ya wanaedelea kupatiwa ushauri nasaha.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com