1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Erdogan atembelea eneo la maafa ya moto

8 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D4DM

LUDWIGSAHAFEN:

Waziri Mkuu wa Uturuki Tayyip Erdogan ametembelea eneo ambako jengo la ghorofa nne liliwaka moto katika mji wa Ludwigshafen kusini-magharibi ya Ujerumani.Wahamiaji 9 raia wa Uturuki walipoteza maisha yao katika moto huo na wengine zaidi ya 60 walijeruhiwa.Erdogan alitoa mwito kwa umma uliokuwa na ghadhabu kubakia shwari na akawasifu wazima moto wa Kijerumani waliokuwa wakikosolewa.Hadi hivi sasa,haijulikani nini kilichosababisha moto huo na tume maalum ya zaidi ya polisi 80 inaendelea kufanya uchunguzi.

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Wolfgang Schäuble amezishutumu ripoti za baadhi ya magazeti ya Uturuki kama ni uchochezi usio na dhamana.Erdogan yupo Ujerumani kwa ziara rasmi iliyopangwa tangu hapo awali kukutana na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na maafisa wengine wa serikali katika mji mkuu Berlin.