1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

England na Uholanzi nani zaidi nusu fainali za EURO 2024?

10 Julai 2024

England inajitupa uwanjani leo usiku kukwaana na Uholanzi katika mchezo wa pili wa nusu fainali ya michuano ya kandanda kwa mataifa ya Ulaya EURO 2024 utakaopigwa kwenye dimba la Signal Iduna mjini Dortmund.

https://p.dw.com/p/4i7JF
Euro 2024: Uingereza - Uswizi
Breel Embolo ya Uswizi akishangilia kuifungia timu yake bao la ufunguzi wakati wa mechi ya robo fainali kati ya England na Uswizi kwenye michuano ya kandanda ya Euro 2024 mjini Duesseldorf, Ujerumani, Julai 6, 2024Picha: Martin Meissner/AP/picture alliance

Vijana hao wa kocha Gareth Southgate wanatumai kufanya maajabu na kutinga fainali ya pili mfululizo baada ya kulikosa chupuchupu kombe la Euro la mwaka 2020. Uholanzi nao wanaitolea macho nafasi ya kucheza fainali na hatimaye kunyakua kombe la kwanza la michuano mikubwa ya kimataifa katika kipindi cha miaka 36.

Mshindi wa mchezo wa leo atakuwa na miadi naUhispaniailiyotangulia fainali hapo jana usiku kwa ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Ufaransa. Fainali za EURO mwa huu zitachenzwa mjini Berlin jumapili inayokuja.