1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Eneo la kuingia Gaza lafungwa

19 Oktoba 2008
https://p.dw.com/p/FcvH

Jerusalem:

Israel leo ililazimika kulifunga eneo moja miongoni mwa yale makubwa kunakopitia bidhaa kuingia ukanda wa Gaza,, wakati waanadamanaji wa Kiisraili walipokusanyika wakidai kuachiwa huru mwanajeshi wa Kiisraili Gilad Shalit anayeshikiliwa na wanaharakjati wa Hamas. Kiasi ya malori 80 yakiwa na vyakula na madawa yalikua yavuke kuingia Gaza lakini yakashindwa kwa sababu ya maandamano hayo.Hamas kinadai kuachiwa huru mamia ya wafungwa wa Kipalestina, ili Shalit aliyekamatwa na huko Gaza wakati wa hujuma za Israel Juni 2006, naye aachiliwe huru.