1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Emmanuel Ramazani Shadary ni nani?

Sekione Kitojo9 Agosti 2018

Mgombea wa kiti cha urais kutoka vuguvugu la vyama tawala nchini Kongo, Emmanuel Ramazani Shadary anaelezewa na watu wa karibu yake kuwa ni mchapa kazi na alie mtiifu kwa rais Joseph Kabila toka mwanzo wa utawala wake.

https://p.dw.com/p/32ugA
Kongo Emmanuel Ramazani Shadary
Picha: REUTERS

Lakini hata hivyo Shadari ni miongoni mwa maafisa wa serikali ya Kongo waliowekewa vikwazo na umoja wau laya kwa kuhujumu haki za binadamu na taratibu ya uchaguzi nchini humo.

Emmanuel Ramazani Shadary mwenye umri wa miaka 57 na ambae atawania kiti cha urais kwa tiketi ya FCC ni miongoni mwa wabunge wazungumzaji sana. Lakini ni kwenye mchakato wa uteuzi wa mgombea wa vyama tawala, wengi hawakumpa uzito wa kuteuliwa.

Ramazani Shadary ambae ni mbunge wa chama tawala cha PPRD toka mwaka wa 2007, alikuwa waziri wa mambo ya ndani na mwaka 1997 alikua gavana wa jimbo la Maniema alikotoka. Mwanasheria huyo wa chuo kikuu cha Lubumbashi ni miongoni mwa watu wanaoaminika kuwa watiifu kwa rais Joseph Kabila. Na uteuzi wake unatokana hasa na ushupavu wake amesema Ferdinand Kambere ambae ni naibu katibu mtendaji wa chama cha PPRD.

Kongo Emmanuel Ramazani Shadary
Mgombea wa kiti cha urais kutoka vuguvugu la vyama tawala nchini Kongo, Emmanuel Ramazani Shadary.Picha: REUTERS

Emmanuel Ramazani Shadary aliongoza tume ya kisheria na kisiasa bungeni na mratibu wa kundi la wabunge wa vyama tawala. Kabla ya kuteuliwa kuwa katibu mtendaji wa chama tawala mapema mwaka huu, Shadari alikuwa miongoni mwa wajumbe saba wa chama tawala walioendesha mazungumzo ya kisiasa na upinzani kwa ajili ya uchaguzi mkuu chini ya uongozi wa kanisa Katoliki.

Hata hivyo wakosoaji wake wamesema kwamba ni mtu anayeghadhibika kwa haraka na ambaye anapenda kila mara msimamo wake upitishwe.

Ramazani Shadary ni miongoni mwa maafisa wa serikali ya Kongo wanaolengwa na vikwazo vya kimataifa vikiwemo vya muungano wa Ulaya. Mashirika ya kutetea haki za binadamu ambayo yamepongeza kutoshiriki kwa rais Kabila kwenye uchaguzi ujao, yamelezea wasiwasi wao kuhusu uteuzi wa Shadary. Georges Kapiamba kiongozi wa shirika la haki za bianadamu la ACCES A LA JUSTICE amesema kwamba wanasubiri kuona utendaji kazi wake ikiwa atachaguliwa.

Ikiwa uchaguzi utafanyika, Kongo itashuhudia kwa mara ya kwanza makabidhiano ya amani ya madaraka.

Mwandishi: Saleh Mwanamilongo.

Mhariri: Sekione Kitojo