Eliud Kipchoge aandika historia | Michezo | DW | 29.04.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Eliud Kipchoge aandika historia

Eliud Kipchoge ameweka rekodi ya kushinda marathon ya London kwa mara ya nne Jumapili. Kipchoge alishinda kwa kuandikisha muda wa 2:02:37, huo ukiwa muda wa pili wa kasi kihistoria katika marathon.

Kipchoge ndiye anayeshikilia rekodi ya kasi zaidi katika marathon baada ya kuandikisha muda wa kasi zaidi duniani alipokimbia kwa 2:01:39 katika marathon ya Berlin, Ujerumani mwaka jana.

Mkenya huyo amekimbia jumla ya marathon 12 na kushinda 11.

Leichtathletik London Marathon | Eliud Kipchoge, Prinz Harry und Brigid Kosgei

Eliud Kipchoge akiwa na mshindi wa kina dada Bridget Kosgei pamoja na mwanamfalme Harry

Muingereza Sir Mo Farah ambaye wengi walitazamia ampe ushindani mkubwa Kipchoge, hakufua dafu na akamaliza katika nafasi ya tano.

Upande wa wanawake bingwa mtetezi Vivian Cheruiyot kutoka Kenya aliishia kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Bridget Kosgei.