1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Elimu kwa wote: Kila mtu ana haki ya kupata Elimu

Mohamed Dahman25 Juni 2012

Jamii ya Kimataifa chini ya muongozo wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO ilikubaliana hapo mwaka 2000 kwamba elimu ni haki ya binadamu. Je, ahadi hii kubwa imetimizwa?

https://p.dw.com/p/14nuB
schwarze Hände mit Buch Projekt: Bildung für Alle
Picha: africa - Fotolia

''Sisi sio Rasilmali Watu-Sisi tunataka Elimu'' tamko hili limeandikwa na wanafunzi wa Uhispania kwenye bango lao wakati walipokuwa wakiandamana mwanzoni mwa mwaka huu kupinga kubinafsishwa kunakohofiwa kwa vyuo vikuu. Claudia Lohrenscheit, mtaalamu katika taasisi ya haki za bindamu nchini Ujerumani, amesema '' ni jukumu la serikali kuzifanya shule na elimu kuwa bure kwa watu wote na misingi yake isiwe ya kiuchumi." Ameitaka serikali katika azimio lake la jumla ihakikishe kutimizwa kwa ahadi ya kumpatia binadamu elimu ikiwa ni kama haki yake ya msingi.

Utekelezaji wa haki za binadamu katika kujipatia elimu sio tu tatizo kwa nchi za kimaskini tu bali pia mataifa tajiri ya magharibi yenye maendeleo makubwa ya viwanda yanakabiliwa na tatizo hilo. Utandawazi unaendeshwa na fedha kama vile inavyoeleza ripoti ya sasa ya Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD na kwamba umeleta mabadiliko duniani kote. Serikali zimekuwa zikijitowa au kurudi nyuma katika masuala ya kuwekeza katika elimu na shughuli hizo zimekuwa zikizidi kubinafsishwa au kufadhiliwa na Makanisa. Lutz Möller wa Tume ya Taifa ya Ujerumani kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO amelibaini hilo.

Serikali lazima ziongoze

Lutz Möller anasisitza kwamba ufadhili wa kibinafsi usiachiwe kuwatenga na kwa hiyo kuwabagua watoto wa wananchi maskini. Anasema '' kwanza itahitajika miundo mizuri ya kiserikali kuandaliwa katika jamii ikiwa na haki za elimu."

Schule; Schüler; Lehrerin; Unterricht; melden; Klassenzimmer; Tafel; Grundschule; Mädchen; lernen; unterrichten; Schulbank; sitzen; strecken; finger; lehren
Mwanafunzi wa shule ya msingiPicha: Fotolia/MAK

Suala la kudai haki za binaadamu haliwezi kutimilizwa katika msimamo wa elimu hususan wenye kutowa kipau mbele kwa uwezo wake wa kufanya kazi. Kwa hiyo elimu inafahamika kwamba ni zana ya kiufundi ambapo binaadamu anatakiwa awe ameandaliwa kuweza kupata kazi katika soko la ajira. Claudia Lohrenscheit wa Taasisi ya Haki za Binadaamu nchini Ujerumani anasema: ''Hiyo ni elimu ambapo kwayo maendeleo ya mtu binafsi hayatiliwi maanani. Kile kilichosomwa husahauliwa kwa haraka sana kinapokuwa hakiwezi kutumika kwa kukosa sifa zinazohitajika katika soko la ajira."

Kushajiisha Maendeleo ya Kibinafsi na Kujiamini

Mwalimu wa Brazil Paulo Freire tayari amebaini hali kama hiyo katika miaka ya 1970 wakati wa kampeni yake ya kufuta ujinga kwa kuboresha hali ya kujuwa kusoma na kuandika. Wakati binaadamu wanajifunza kusoma na kuandika hawapati fursa ya kulitumia hilo kwa ajili ya kuboresha hali yao ya maisha na kwa hiyo kwa mara nyengine tena wanakuwa wanapoteza ujuzi wao. Elimu ina maana iwaongoze na hususan katika hali ya kujiamini kuboresha hali yao ya maisha.

Näherin, berufsbildende Schule in Sake, Ruanda Coyright: Hanne Hall / Innenministerium Rheinland-Pfalz
Mshonaji wa Chuo cha Ufundi wa Sake, RwandaPicha: Innenministerium Rheinland-Pfalz

Venginevyo mtaalamu huyo wa haki za binaadamu Claudia Lohrenscheit anasema katika hitimisho lake kwamba watu huachana na madai yao ya haki ya kupatiwa elimu.

Ni wajibu wa Jumuiya ya Kimataifa kuhakikisha kutumika kwa fikra za elimu. Kwa hiyo kipau mbele lazima kiwe katika kuboresha haki ya binadamu kujipatia elimu kwa wale wanaoishi kwa mfano kwenye umaskini,wanaotengwa au kwenye sehemu za vita na mizozo.

Kwa mujibu wa Claudia Lohrensscheit kuwapa fursa ya elimu watu dhaifu kama hao "kutapima kiwango cha ustaarabu na pia maendeleo ya binadamu katika jamii.''

Kuwezesha Watu Kupata Elimu

Shauku ya mjumbe wa zamani wa Umoja wa Mataifa aliekuwa akirepoti juu ya haki ya elimu Katharina Tomaschevski ilikuwa ni suala la kuyakinishwa kwa mahitaji ya haki ya kupatiwa elimu. Alitengeneza muongozo wa vigezo vinne ambavyo vyote vimeanzia na herufi A.

Teil des Projekts in Sarwan ist auch mehr Kinder eine Schulbildung zu ermöglichen. Beim Projektstart besuchte in Sarwan weniger als jedes dritte Kind eine Schule. Foto: Helle Jeppesen/DW, eingepflegt: Oktober 2010
Picha hii inaonyesha wanafunzi wa Sarwan. Lengo la mradi wa Sarwan ni kuboresha upatikanaji wa elimu kwa watoto.Picha: DW

Kwanza ni 'Avalability' yaani uwepo wa elimu.

Pili ni 'Accessability' yaani upatikanaji wa elimu.

Tatu ni 'Adaptability' yaani kuoana na elimu.

Na nne ni 'Acceptability'  elimu inayokubalika yaani aina ya elimu yenye kuzingatia haki za binadamu. 

Hususan katika nchi za kimaskini duniani mara nyingi watu wamekuwa wanashindwa kupata elimu kwa mfano katika vijiji kunakuwako choo kimoja tu katika shule ambacho inabidi kitumiwe kwa pamoja kati ya wavulana na wasichana jambo ambalo halikubaliki kitamaduni na kiafya na huwafanya wasichana kutokwenda shule. Hayo yameripotiwa na mtaalumu wa haki za binaadamu Lutz Möller kutokana na uzoefu wake akiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Ulimu, Sanyasi na Utamaduni UNESCO kwenye nchi nyingi nyingi zinazoendelea duniani.

Kuhakikisha Upatikanaji wa Elimu ya msingi na ilio bora

Umoja wa Mataifa hapo mwaka 2000 iliandaa Kongamno la Elimu mjini Dakar Senegal kuboresha fursa za elimu. Nchi 164 zilizungumzia malengo sita ya elimu ambapo kwayo kufikia mwaka 2015 watoto wote wanatakiwa wawe wamepatiwa elimu ya msingi hata hivyo hadi sasa watoto milioni 70 wenye umri wa kwenda shule ya msingi hawapatiwi elimu. Matatizo zaidi yako hasa Asia ya Kusini Masharki, Asia ya Kusini na eneo la kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika. Kwa upande mwengine Möller amepongeza kile alichosema kuwa ni mafanikio yaani kuongezeka kwa idadi ya wanawake wanaopata elimu ya msingi kulinganisha na ile ya ya wanaume.

Bilder hier zeigen eine Schule mit rund 1.000 Schülern, die World Vision mit Unterstützung der Telekom in dem stark anwachsenden Stadtteil Corail erbaut hat. Viele dieser Kinder leben in den Übergangshäusern, manche auch noch in Zelten. Quelle World Vision
Wanafunzi wa shule iliyojengwa kwa msaada wa Shirika la World Vision na Telekom katika mtaa wa Corail, HaitiPicha: World Vision

Changamoto kubwa inayoikabili UNESCO ni ubora wa elimu: Walimu wenye ujuzi milioni mbili wanaume na wanawake wanahitajika duniani kote, madarasa bado yana wananfunzi wengi kupindukia na vifaa vya shule ikiwa ni pamoja na vitabu na vifaa vya kuandikia lazima viboreshwe. UNESCO imelitilia mkazo jambo hilo katika repoti yake kuhusu elimu mwaka 2011 na imezitaka nchi zenye kutowa mikopo kupeleka misaada ya kifedha kwa nchi hizo za kimaskini. Lutz Möller anasema mbali na hayo fikra za elimu za taifa lazima ziimarishwe zaidi kipindi cha usoni, mada hiyo iwe endelevu na kuimarisha mawasiliano na wazazi watarajiwa juu ya namna ya kutumia rasilmali za dunia zinazozidi kupunguwa. 

Kuendeleza Demokrasia na lengo la Elimu

Haki ya binaadamu kujipatia elimu na kutaka kufanikisha kuishi kwa pamoja kwa amani na bila ya ubaguzi kwenye jamii inayodelea kongezeka ni jukumu la mataifa yote. Kwa Claudia Lohrenscheit ni muhimu kuwaangalia watu wazima na kuwashajiisha waendelee kujifunza maisha. Haki ya binadamu kupata elimu itatimizwa hususan kwa ubora wa elimu wakati mamlaka ya watu kujiamulia mambo yao yatakapoimarishwa, waweze  kushughulikia na kusimamia wenyewe maisha yao kikamilifu. ''Kila binadaamu ana haki ya kujipatia elimu na hiyo kujiendeleza kibinafsi kwa kujifunza na kuheshimu haki za binaadamu na misingi ya uhuru".

Autorin: STRATO AG Berlin Ort: Ein Raum im Instituto Industrial de Maputo. Datum: Oktober 2011 Bildbeschreibung:Auf dem Foto befinden sich Schüler des Projektes Mosambit, im Instituto Industrial de Maputo. Das Bild wurde im Oktober 2010 gemacht, als die Planung für das Projekt MoçamBIT bei STRATO entstand. Das Foto zeigt NICHT das von STRATO eingerichtete Computerlabor, sondern Schüler in einem Raum im Instituto Industrial de Maputo.
Wanafunzi wa mradi wa Mosambit, Instituto Industrial de Maputo, MsumbijiPicha: Strato AG

Mwandishi: Mast-Kirsching, Ulrike/ Mohamed Dahman

Mhariri: Bruce Amani