El baradei akutana na Ayatoullah Khamenei wa Iran. | Habari za Ulimwengu | DW | 13.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

El baradei akutana na Ayatoullah Khamenei wa Iran.

Tehran.

Mkuu wa shirika la kimataifa la nishati ya atomic Mohammed El Baradei amekutana na kiongozi wa kidini nchini Iran Ayatoullah Khamenei kwa mazungumzo juu ya mpango wa nchi hiyo wa kinuklia. Katika mkutano huo, Khamenei amemweleza El Baradei kuwa Iran haitaacha kile alichokieleza mpango wake wa kinuklia wa amani. Amesema kuwa Marekani haitaweza kuipigisha magoti Iran, na kuongeza kuwa jalada la kinuklia la Iran linapaswa kushughulikiwa na shirika hilo la kimataifa la nishati ya Atomic na sio baraza la usalama la umoja wa mataifa. Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeweka vikwazo mara mbili dhidi ya Iran kutokana na kushindwa kwake kuweka wazi maelezo yote ya kazi zake nyeti za kinuklia. El Baradei pia amekutana na rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad , ambaye amemtaka kiongozi huyo kuzuwia mbinyo wa Marekani na kubaki katika msimamo wa kati. Kiongozi huyo wa IAEA ameutaka uongozi wa Iran kuongeza ushirikiano na uwazi zaidi. Mataifa ya magharibi yanashaka kuwa taifa hilo la Kiislamu linataka kuunda silaha za kinuklia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com