EL-ARISH:Wahamiaji 10 wafyatuliwa risasi Sinai | Habari za Ulimwengu | DW | 14.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

EL-ARISH:Wahamiaji 10 wafyatuliwa risasi Sinai

Polisi nchini Misri waliwafyatulia risasi wahamiaji 10 walioa na asili ya Kiafrika waliokuwa wakijaribu kuingia nchini Israel bila vibali.Wanne kati yao walikamatwa na wengine sita walibahatika kupenya na kuingia Israel kwa mujibu wa afisa mmoja wa usalama wa Sinai ambaye hakutaka jina lake kufahamika.Bado haijulikani iwapo wahamiaji hao 6 walijeruhiwa na risasi.Watatu kati yao wanaripotiwa kutokea nchi ya Eritrea,mmoja wa Sudan na mwengine wa Ivory Coast.Wahamiaji haramu wanaotokea Misri na kuingia Israel wanasababisha mvutano kati ya mataifa hayo mawili jambo linaloifanya serikali ya Israel kuishinikiza Misri kuimarisha usalama katika mpaka wake.

Wahamiaji hao wa Eritrea wanaripotiwa kumlipa msafirishaji mmoja wa magendo euro 706 kuwaingiza katika rasi ya Sinai na kuwasaidia kuingia Israel kulingana na afisa huyo wa usalama wa Sinai.Kulingana na takwimu za Israel wahamiaji haramu 2800 wameingia nchini humo wakitokea Misri wengi wao wakiwa na asili ya kiAfrika.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com