DW yatimiza miaka 65
Tangu DW ilipoanza kurusha matangazo yake kimekuwa chanzo cha kuaminika cha habari zinazohusu ulimwengu mzima.
Idhaa ya Kiswahili ya DW miaka ya 1970
Wafanyakazi na watangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle wakichagua barua kwenye sanduku la kupokelea barua za wasikilizaji katika miaka ya 1970.
Idhaa ya Kiswahili ya DW miaka ya 1960
Timu ya Idhaa ya Kiswahili ya Deutche Welle katika miaka ya 1960, siku hizo ikijuilikana kwa jina la Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani.
Idhaa ya Kiswahili ya DW miaka ya 1970
Timu ya Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle katika miaka ya 1970. Miongoni mwao, kutoka kushoto, ni Mohammed Abdulrahman na Prema Martin, na kutoka kulia ni Ramadhani Ali na Othman Miraji.
Ushirikiano wa DW na Idhaa nyengine za kimataifa
Naibu wa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Hans Koeppel, akizungumza kwenye kongamano la vyombo vya habari na afya lililoandaliwa kwa ushirikiano wa DW na Idhaa nyengine za kimataifa jijini Dar es Salaam, Tanzania, Mei 2012.
Eva-Klau Machangu alipoagwa kwenye miaka ya 2000
Kadi maalum ya kumuaga mmoja wa wafanyakazi wa muda mrefu wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle, Eva-Klau Machangu, kwenye miaka ya 2000.
John Kanyunyu, Goma DRC
Mwakilishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, John Kanyunyu (kushoto) akiwa kazini.
Alfred Kiti, DW Nairobi
Mwakilishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle nchini Kenya, Alfred Kiti (kushoto), akiwa kazini
Noa Bongo Jenga Maisha, 2009
Kutoka kushoto: Johannes Becker wa Idhaa ya Kireno, mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili Zainab Aziz na mkuu wa Idhaa ya Kiswahili Andrea Schmidt katika sherehe za Tuzo ya Noa Bongo, Jenga Maisha mwaka 2009.
DW Kiswahili na msaada kwa albino Tanzania
Aboubakar Liongo wa Idhaa ya Kiswahili ya DW akikabidhi mipira kwa timu ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Tanzania mwaka 2008, ikiwa ni sehemu ya shughuli za kijamii za DW.
Idhaa ya Kiswahili ya DW 2009
Kutoka kushoto: Halima Nyanza, Thelma Mwadzaya na Andrea Schmidt wakiwa kwenye mkutano wa kupanga matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW mwaka 2009.
Sekione Kitojo, DW 2013
Sekione Kitojo akiwa kazini kwenye matangazo ya moja kwa moja katika studio za DW Bonn.
Amina Abubakar, DW 2013
Tunaamini katika ufanisi na umakini wa kazi zetu. Amina Abubakar akiwa kazini kwenye studio za DW Bonn
Wakongwe na wapya, DW 2013
DW Kiswahili sio tu kwamba ni redio ya kutangazia wasikilizaji wake, bali pia taasisi ya kuwatayarisha wafanyakazi wake, ambapo wazoefu huchangia mawazo na wanagenzi ili kurithishana ujuzi na maarifa. Samia Othman (kushoto) na Bruce Amani.
DW Kiswahili na redio washirika
Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili, Andrea Schmidt (katikati) akiangalia namna moja ya redio washirika wa DW inavyorusha moja kwa moja matangazo yetu kwa wasikilizaji wa Tanzania.
DW, Dar es Salaam
DW nje ya DW. Kwa kuzingatia umuhimu wa elimu na mafunzo katika ufanikishaji wa kazi zetu, daima tumekuwa tukishirikiana na wenzetu kote Afrika Mashariki na Kati kuhakikisha lengo hilo linatimizwa. Warsha ya Idhaa ya Kiswahili kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Tunavuma kwa kishindo
Tunavuma kwa kishindo! Kijana huyu anakula ugali wake huku akisikiliza matangazo ya mchana ya Idhaa ya Kiswahili kupitia redio yake katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam.
Mohammed Abdulrahman DW
Mohamed Abdulrahman wa Idhaa ya Kiswahili ya DW akimfanyia mahojiano maalum aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Burundi, Simon Nyandwi.
DW Nairobi
Mkuu wa zamani wa Idhaa ya Kiswahili, Ben Wazir (kushoto waliokaa jukwaani), akitoa mada kwenye mjadala wa dhima ya vyombo vya habari vya kimataifa katika lugha ya Kiswahili jijini Nairobi mwaka 2008.
Matangazo yakipelekwa hewani
Mti ni nyenzo! Kuifanya sauti ya watangazaji isikike kwenye redio kwa wakati na kwa mpangilio unaostahiki ni kazi kubwa, na nyuma ya kazi hiyo kuna Nina Markgraf (kushoto), muongozaji wetu wa matangazo.
Bado kijana mbichi!
Mchoro huu uliotumwa na Shaaban Manyanga wa Dar es Salam, Tanzania, ulikuwa sehemu ya mashindano ya Miaka 50 ya Idhaa ya Kiswahili ya DW (mwaka 2013).
Teknolojia, utamaduni na mawasiliano
Teknolojia, utamaduni na mawasiliano, yote kutoka DW. Mchoro huu umechorwa na Khalid Maulid Saburi wa Dar Art Youth, Dar es Salaam, Tanzania, kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 50 ya Idhaa ya Kiswahili (mwaka 2013).
DW kazini
Vipawa huzaliwa, lakini uwezo hujengwa. Abdu Mtullya (kulia) akichangiana maarifa na ujuzi wake na watangazaji wapya Grace Kabogo (katikati) na Stumai George.
Nuru katikati ya giza!
Mchoro wa Fredrick Yustard Ngimbwa kutoka Dar es Salam, Tanzania kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Idhaa ya Kiswahili ya DW (mwaka 2013).
Walioijenga DW
Mkuu wa zamani wa Idhaa ya Kiswahili ya DW, Ben Wazir, ni miongoni mwa watu walioijenga Idhaa hii kuwa moja ya redio bora duniani.
Sauti iliyokamilika
Saumu Mwasimba, mmoja wa watangazaji wanaoifanya Idhaa ya Kiswahili ya DW kuendelea kuvuma kwa kishindo.