DUSHANBE.Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumai amefanya mazunguzmo na rais wa Tajikstan | Habari za Ulimwengu | DW | 03.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DUSHANBE.Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumai amefanya mazunguzmo na rais wa Tajikstan

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank- Walter Steinmier akiwa katika ziara ya nchi za Asia ya kati leo amefanya mazungumzo na rais Emomali Rahmonov wa Tajikstan katika mji mkuu wa Dushanbe.

Steinmier amemtaka rais Rahmonov kutilia mkazo mabadiliko katika katiba ya nchi hiyo ili kutoa nafasi ya maendeleo ya kisasa kwa jamii ya Kyrgystan.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmier baadae anatarajiwa kuzuru Krygystan ambako maelefu ya waandamanaji katika mji wa Bishkek wameapa kuendelea kumshinikiza kiongozi wa nchi hiyo Kurmanbek bakiyev ajiuzulu.

Maandamano hayo yalianza jana nchini Kyrigystan baada ya rais Bakiyev kushindwa kuwasilisha mabadiliko ya katiba yenye kifungu kinacho mpunguzia uwezo katika mamlaka yake ya urais.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com