1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Duru ya pili ya uchaguzi wa urais Serbia Febuari 3

21 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CvZC

BRUSSELS:

Umoja wa Ulaya umehakikisha imani yake kuimarisha uhusiano wake na Serbia kufuatia duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais.Mmoja wa wagombinia urais na mwenye siasa kali za kizalendo –Tomislav Nikolic amepata asili mia 39.6 ya kura katika duru ya kwanza ya jumapili mbele ya mwenzake rais Boric Tadic anaeegemea nchi za magharibi aliepata asili mia 35.5 ya kura.Tadic amesema kuwa hana shaka mkondo wa Serbia kuelekea umoja wa Ulaya utaimarishwa.

Tadic na mwenzake Nikolic watapambana tena katika duru ya pili itakayofanyika mwezi febuari 3. Hata hivyo leo jumatatu mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya-Javier Solana amesema kuwa Umoja wa Ulaya unaimani kuwa Serbia itachapuza juhudi za nchi hiyo kuelekea umoja wa Ulaya.Uchaguzi wa Serbia,umekuja wakati wa kipindi kigumu.Hali ya wasiwasi inaongezeka kuhusu siku za mbele za jimbo la Kosovo.