DUBAI: Tawi la al-Qaeda lajitambulisha na shambulizi jipya | Habari za Ulimwengu | DW | 22.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DUBAI: Tawi la al-Qaeda lajitambulisha na shambulizi jipya

Tawi la Al-Qaeda katika Afrika ya Kaskazini limesema kuwa limehusika na shambulizi la kujitolea muhanga la siku ya Ijumaa,nchini Algeria.Msafara wa magari ulishambuliwa mashariki ya mji mkuu Algiers.Mripuko huo ulijeruhi Waalgeria 6,Wafaransa 2 na Mtaliana mmoja.

Mwanzoni mwa mwezi huu pia,tawi la Al-Qaeda la Afrika ya Kaskazini,lilijitambulisha kuhusika na mashambulizi mengine mawili nchini Algeria. Mashambulizi hayo yaliua zaidi ya watu 50.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com