DUBAI: Naibu kiongozi wa al Qaeda atishia kuichukulia hatua Uingereza | Habari za Ulimwengu | DW | 11.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DUBAI: Naibu kiongozi wa al Qaeda atishia kuichukulia hatua Uingereza

Naibu kiongozi wa al- Qaeda, Ayman al Zawahri, ametishia kwamba kundi lake linajiandaa kuchukua hatua dhidi ya uamuzi wa Uingereza kumtunza heshima ya ubwana yaani Knighthood, mwandishi wa vitabu, Salman Rushdie.

Kwenye ujumbe wake katika ukanda wa video uliotumwa kwenye tovuti moja ya wanamgambo wa kiislamu, al Zawahri aliishutumu Uingereza kwa kuwa na unafiki kwa kumpa heshima hiyo Rushdie ikisingizia kuenzi uhuru wa kujieleza.

Rushdie anashutumiwa na baadhi ya waislamu kwa kuutukana uislamu kwenye kitabu chake cha aya za shetani, ambacho kilizusha kashfa kubwa ya kimataifa wakati kilipochapishwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka wa 1988.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com