DRESDEN:Rais Putin wa Urusi aendelea na ziara nchini Ujerumani | Habari za Ulimwengu | DW | 11.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DRESDEN:Rais Putin wa Urusi aendelea na ziara nchini Ujerumani

Rais Vladmir Putin wa Urusi anaendelea na ziara nchini Ujerumani amekutana na mwenyeji wake Kansela Angela Merkel katika mji wa Dresden mashariki mwa Ujerumani.

Katika mazungumzo yao viongozi hao walijadili masuala ya mashariki ya kati,nishati na biashara baina ya nchi zao.

Rais Putin pia alizungumzia juu ya mwandishi habari mashahuri wa Urusi Anna Politkovskaya alieuawa mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Moscow.

Bwana Putin amewaambia wandishi habari kwamba mauaji hayo ni uhalifu wa kikatili na kwamba waliotenda lazima waadhibiwe.

Mwandishi huyo aliezikwa jana na maalfu ya watu mjini Moscow aliuliwa kwa sababu ya makala alizokuwa anaandika kufichua matendo dhalimu ya majeshi ya Urusi nchini Chechnya.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com