1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRESDEN.Angela Merkel anatarajia kuchaguliwa tena kukiongoza chama cha CDU

27 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCp5

Mkutano mkuu wa chama cha Christian Democratic Union (CDU) unaendelea mjini Dresden mashariki mwa Ujerumani ukikabiliwa na mzozo juu ya mwelekeo wa chama hicho katika siku za usoni pamoja na kupungua umaarufu.

Mwenyekiti wa sasa wa chama hicho anaetarajiwa kuchaguliwa tena kushika wadhifa huo kansela wa Ujerumani Angela Merkel leo anatazamiwa kusisitiza kuwa CDU ni chama cha umma.

Baadhi ya wanachama wa ngazi za juu wanataka chama hicho kiweke mkazo katika sera za kijamii wakati wengine wanapinga hoja ya kukifanya chama hicho kielekee mlengo wa kushoto.

Katika hotuba yake bibi Merkel anatarajiwa kusisitiza kuwa chama cha CDU ni chama cha mlengo wa kati chenye mikondo tofauti inayojumuisha maadili ya kikristo, uhuru wa kiuchumi na uhafidhina.

Vyama ndugu vya kihafidhina vya CDU na Christian Social Union vinaunda serikali ya mseto na chama cha Social Democratic SPD.