Dortmund yaicheweshea Bayern ubingwa Bungesliga | Michezo | DW | 12.05.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Dortmund yaicheweshea Bayern ubingwa Bungesliga

Kinyang'anyiro cha kuwania taji la Ligi Kuu ya Ujerumani - Bundesliga kimekwenda hadi siku ya mwisho baada ya wanaotegemewa kushinda Bayern Munich kuvutwa shati la Leipzig huku Borrusia ikipata ushindi.

Borussia Dortmund - Fortuna Düsseldorf (picture-alliance/dpa/B. Thissen)

Borussia Dortmund walifufua matumaini yao ya ushindi kwa kuifunga Fortuna Düsseldorf mabao 3:2, Mei 11, 2019.

RB Leipzig 0-0 Bayern Munich

Borussia Dortmund 3 - 2 Fortuna Düsseldorf

(Pulisic 41', Delaney 53', Götze 90+2' - Fink 48', Kownacki 90+5, Bodzek s/o 81')

Bayern Munich ilikosa nafasi ya kushinda taji lake la saba mfululizo kwenye Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga, baada ya kuvutwa shati na klabu ya RB Leipzig huku mahasimu wao Dortmund waking'angana kwa bidii kuchukuwa pointi zote tatu nyumbani dhidi ya timu iliyoko nafasi ya kati ya Fortuna Düsseldorf.

Leon Goretzka alidhani ameipa Bayern ubingwa wa Ligi kwa goli la kipindi cha kipindi cha pili, lakini refa msaidizi wa video alilikataa bao hilo kwa kuotea, wakati ambapo kinyang'anyiro cha ubingwa kikisalia bila mshindi wa wazi.

Dakika kadhaa kabla, katika upande wa pili wa nchi, mlinda mlango wa akiba wa BVB Marwin Hitz alifanya kosa kubwa wakati klabu yake ilipofungwa bao la kusawazisha na Oliver Fink baada ya Christian Pulisic kuifungia Dortmund goli lake la mwisho la nyumbani kwa kichwa safi.

Wakati Bayern wakiharibu nafasi yao, Thomas Delaney alirejesha uongozi wa Dortmund katika dakika ya 53 kwa mkwaju mzito, baada ya juhudi zake za awali kuzuiwa, kabla ya Hitz kukaribia kuigharimu timu yake kwa mara nyingine, kwa kufungwa mkwaju wa penati muda mfupi tu kabla ya saa moja ya mchezo. Lakini mpira wa Dodi Lukebakio ulikwenda nje ya lango.

Fußball Bundesliga RB Leipzig - Bayern München (Getty Images/AFP/O. Andersen)

Bayern Munich ililaazimishwa sare ya 0-0 na RB Leipzig na kukosa nafasi ya kufunga taji lake la saba mfululizo.

RB Lepzig yaiwiwa kisiki Bayern

Wakati huo huo, kipaji cha mashambulizi kilichoonyeshwa mjini Leipzig kilikuwa na athari kidogo kwenye mechi, ingawa nafasi kubwa zaidi ziliiangukia Bayern. Si Serge Gnaby wala Robert Lewandowski waliweza kuzitumia.

Marcel Halstenberg alikuwa na nafasi mbili za kuifungia RB wakati kipindi cha pili kikikaribia lakini hakumpa shida yoyote Sven Ulreich, huku Serge Gnaby akigonga mwamba kwa Bayern - ingawa pia alikuwa ameotea.

Lakini kishindo cha Bayern kilikuwa kinaongezeka. Frank Ribery aliingia na kugonga mpira wa Thomas Mueller kwenye box kuelekea langoni lakini Gulacsi aliokoa tena kwa karibu, kabla ya Lewandowski kukosa mpira wa adhabu wakati ambapo RB ikishikilia.

Licha ya juhudi murua za Mario Gätze katika muda wa majeruhi zilizoipandisha Dortmund 3-1, na kuodolewa kwa Adam Bodzek katika dakika za mwisho, BVB ilikaribia kutupa ushindi wake.

Dawid Kownacki alipatiwa nafasi kwenye boksi na kufunga bao na kusababisha mhemko kwenye boksi la Dortmund.

Lakini walifanikiwa kusalia hai kwa wiki nyingine, na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa kinyang'anyiro hiki cha kuvutia zaidi katika kipindi cha miaka kadhaa.

Mshindi wa taji hilo ataamuliwa wiki ijayo, wakati Dortmund itakaposafiri kwenda Borrusia Moenchengladbach ikihitaji ushindi, huku ikitumai kuwa Eintracht Frankfurt itashinda mjini Munich.

vyanzo: dw