1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DONETSK : Mripuko wa gesi wauwa 65 katika mgodi

19 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CIli

Takriban wafanyakazi wa migodi 65 wameuwawa kutokana na mripuko gesi kwenye mgodi wa makaa ya mawe nchini Ukraine.

Waokozi wanawatafuta wafanyakazi wengine 35 ambao bado hawajulikani walipo.Kulikuwa na zaidi ya watu 450 waliokuwa wakifanya kazi ndani ya mgodi huo wa Zasyadko wakati ulipotokea mripuko huo hapo jana katika mkoa wa mashariki wa Donetsk.

Mgodi wa Zasyadko mojawapo ya migodi mikubwa kabisa nchini Ukraine unaajiri takriban watu 10,000 na huzalisha tani 10,000 za makaa ya mawe kwa siku.