1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dola 900,000 za misada zaibiwa huko nchini Kongo

7 Juni 2023

Shirika moja la misaada lenye makao yake makuu nchini Marekani, GiveDirectly, limesema kuwa takribani dola laki 900,000 ziliibiwa kutoka katika programu zake za nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4SI1v
Felix Tshisekedi Präsident DR Kongo
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Antoine TshisekediPicha: Isa Terli /AA/picture alliance

Shirika hilo limesema katika taarifa yake kwamba wizi huo ulifanywa na wafanyakazi wa ndani wa shirika hilo kwa kushirikiana na watu wa nje.

Zaidi ya familia 1,700 maskini ambazo zilihitaji misaada zimeathirika na wizi huo uliotendeka kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita kuanzia mwezi Agosti mwaka 2022.

Uchunguzi unafanyika ili angalau kurejesha sehemu ya fedha hizo ingawa kiasi kikubwa cha pesa hiyo huenda kisipatikane.

Shirika la GiveDirectly hutoa misaada kupitia teknolojia ya miamala ya kwenye simu, ambayo linasema kuwa inaepuka aina nyingi za wizi. 

Eneo la mashariki mwa Kongo ambako shirika hilo linafanya kazi, limekumbwa na mzozo kwa miongo kadhaa.