´Dmitry Medvedev aahidi kufuata nyayo za Putin | Habari za Ulimwengu | DW | 03.03.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

´Dmitry Medvedev aahidi kufuata nyayo za Putin

-

MOSCOW

Rais mteule wa Urussi Dmitry Medvedev ameahidi kuendeleza sera za Vladmir Putin ikiwwemo kutetea maslahi ya Urussi katika ulingo wa kimataifa.Kauli hiyo ameitoa baada ya kushinda uchaguzi wa rais uliofanyika jana ambao wakosoaji wanasema ulipangwa kwa njia za kuhakikisha bwana Putin anabakia kuwa mwenye usemi nchini humo.Medyedev alitangazwa na tume ya uchaguzi kuwa mshindi kwa kupata asilimia 70 ya kura zote zilizopigwa.Medvedev mwenye umri wa miaka 42 ambaye alikuwa zamni ni wakili na kufanya kazi kwa karibu na bwana Putin tangu miaka ya tisini ataapishwa ramsi kama rais mpya wa Urussi katika sherehe itakayofanyika tarehe 7 mwezi May.Putin ambaye kisheria hakuruhusiwa kugombea tena wadhifa huo wa rais atakuwa ni waziri mkuu katika serikali mpya.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com