DIYARBAKIR:Watu 12 wauawa huko Uturuki katika shambulizi la kushtukiza | Habari za Ulimwengu | DW | 30.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DIYARBAKIR:Watu 12 wauawa huko Uturuki katika shambulizi la kushtukiza

Watu 12 wameuawa katika mji wa Diyarbakiri uliyoko katika mpaka wa Iraq na Uturuki, baada ya waasi wa Kikurd kufanya shambulizi la ghafla dhidi ya basi moja dogo.

Maafisa wa jeshi la Uturuki wamesema kuwa miongoni mwa waliyouawa ni pamoja na walinzi wa kijiji kilichoko kwenye mpaka huo, ambao walikuwa kwenye harakati zilizoanza katikati ya mwezi huu kupambana na waasi waliyojitenga kutoka chama cha Kurdistan Workers Party.

Shambulizi hilo limefuatia kuawa kwa afisa wa juu wa waasi hao, waliyoanza harakati zao mwaka 1984 za kutaka kujitangazia uhuru wa eneo la kusini mashariki mwa Uturuki.

Zaidi ya watu elfu 30 wamekwishauawa mpaka sasa kutokana na mzozo huo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com