1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DIYALA:Viongozi wa kisuni wauawa nchini Irak

10 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBKH

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga aliekuwa amevaa kizibau kilichojaa mabomu ameua viongozi watano wa kisuni katika jimbo la kati la Irak Diyala. Polisi imesema mtu huyo alijilipua wakati wa mkutano wa viongozi wa jimbo hilo.

Waliouawa walikuwa wajumbe wa baraza la ukombozi lilioundwa katika jimbo la Diyala ili kupambana na al-kaida katika sehemu hiyo.