Dimba la wanaume la Olimpik leo | Michezo | DW | 08.08.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Dimba la wanaume la Olimpik leo

Alhamisi ni zamu ya dimba la wanaume :Brazil ina miadi na Ubelgiji na Argentina na Ivory Coast.

Ingawa mwenge wa olimpik umeshawasili Beijing na kesho utawaka katika uwanja wa olimpik wakati wa sherehe za ufunguzi, firimbi ililia jana kwa changamoto za dimba la Olimpik.Timu 2 zilicheza finali ya Kombe la dunia mwaka jana nchini China-Ujerumani na Brazil zilifungua dimba na kuachana suluhu 0:0.

Leo ni zamu ya dimba la akina kaka ambamo pia kama la akina dada ,Brazil inaazimia kutamba na kuvaa taji. Timu 3 za Afrika zimo katika mashindano haya ya timu za wanaume na mbili tayari ni mabingwa wa Olimpik-Nigeria na kamerun.Timu ya tatu ni Ivory Coast ambayo inacheza leo na Argentina,ilionyimwa stadi wake wa FC Barcelona Lionel Messi kufuatia uamuzi wa Mahakama ya spoti iliozima amri ya FIFA.

►◄

Mahakama ya michezo iliosikiliza kesi ya vilabu kadhaa vya ulaya kama FC Barcelona ya Spian au Bremen na Schalke za Ujerumani zilizogoma kuwaruhusu wachezaji wao kama Diego na Messi kucheza katika dimba la Olimpik, imetoa hukumu kuzipa haki klabu hizo.Swali sasa ni je, zitawarudisha katika klabu zao mastadi hao ambao tayari kama vile Ronaldinho wa AC milan na Diego pamoja na Messi wako China ?

Shaka shaka zlikua juu ya lionel Messi kuwa angeukosa mpambano wa leo na Tembo wa Ivory Coast. Taarifa nyengine zilisema atabakia kucheza.

Ronaldinho ambae jana alimuangalia stadi mwenzake wa kike Marta akisakata dimba katika timu ya wanawake wa Brazil iliotoka suluhu 0:0 na ya Ujerumani,ameitaja Argentina kuwa kitisho kikubwa kwa ushindi wa Brazil katika dimba hili la Olimpik.Ronaldinho,mwenye umri wa miaka 28 ni mmoja kati ya turufu za kocha dunga wa Brazil katika dimba la olimpik.Klabu yake mpya ya AC Milan imetoa ridhaa yake kumuachia Ronaldinho kutamba katika olimpik leo huko She nyang inakocheza na Ubelgiji.

Katika kundi A la Argentina na Ivory Coast , zinacheza pia Australia na Serbia.

Kundi B linajumuisha Japan inayocheza na Marekani na Holland yenye miadi leo na Nigeria.

Timu ya kike ya Nigeria ilizabwa jana bao 1:0 na Korea.Nigeria, ndio mabingwa wa 1996 wa olimpik walipocheza na akina Nwanko Kanu.

Kundi D linalocheza huko Qinhuangdao ni kati ya Hondurus wenye miadi na Itali wakati simba wa nyika-kamerun -mabingwa wa Sydney, 2000 wanapambana na korea ili kuwalipizia kisasi wasichana wa Nigeria, waliotimuliwa jana kwa bao 1:0 na wakorea.

Ikiwa Brazil itashinda kundi lake katika duru hii pamoja na ile ya robo-finali wamepangwa kuonana na mahasimu wao argentina,timu kali kabisa inayopanga kuwapelekea salamu leo wakicheza na corte d'iviore.

hukumu ya jana ya mahkama ya spoti inawaathiri wabrazili wengine 2-Diego wa Werder Bremen na Rafinha wa Schalke. haifahamiki pia iwapo timu zao zitan'gan'gania kuwarudisha kambini tayari kwa msimu wa Ligi kuanza.

Baada ya changamoto za leo za dimba, macho yote yatakodolewa uwanja mkuu wa olimpik -jumba la ndege-mjini Beijing,kujionea ufunguzi rasmi wa michezo ya 29 ya olimpik ya kisasa.Jumla ya marais na viongozi wa serikali 80 watazamiwa hapo kesho kuhudhuria.Pamoja nao ni Rais George Bush wa Marekani alietembelea jana Korea ya kusini na baadae Thailand.

Baada ya wiki kadhaa za siasa na maandamano,macho ya mashabiki yatakodolewa kuanzia kesho katika Olimpik yenyewe.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com