Dimba la AFCON kuendelea kama ilivyopangwa | Michezo | DW | 04.11.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Dimba la AFCON kuendelea kama ilivyopangwa

Shirikisho la Soka Barani Africa CAF limesema michuano ya Kombe la Soka la Mataifa itaendelea kama ilivyopangwa licha ya kuwepo kitisho cha maradhi ya Ebola

CAF-Präsident Issa Hayatou in Marokko

Rais wa Shirikisho la Kandanda Afrika - CAF, Issa Hayatou

Pia Shirikisho hilo limeipa Morocco muda wa hadi Jumamosi wiki hii kukubaliana na ratiba ya mashindano hayo, na ikishindwa kufanya hivyo itapoteza nafasi ya kuwa mwenyeji.

Baada ya mkutano wa kamati yake kuu mwishoni mwa juma lililopita, kamati hiyo ilikutana na maafisa wa Morocco ambao wanataka michuano hiyo iahirishwe. Uamuzi wa CAF iwapo Morocco itaandaa mashindano hayo au la utatolewa mwishoni mwa juma hili.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Abdul-rahman